Sehemu ya Kuwepo!
30 Sep
Mfalme wa rhymes kutoka morogoro muite afande selle amesema Mkubwa fella kutoka pande za kiumeni amekua akimchukia toka zamani kwani kila afande anapofanya show na wanaume amekua akizima mic lil saut ya afande isisikike fresh na vitu kibao vyenye nia ya kumpoteza mfalme katika game,MKUBWA FELLA alipatikana hewani na kuweza kujibu mashtaka hayo.MKUBWA alisema hajawai kufanya vitu kama hivyo kwakua ye hana muda wa kujenga chuki na mtu ila mda aliokua nao ni wakuangali wasanii wake na kuhakikisha wanafanya vizuri na si kama anavyosema afande
29 Sep
Safari haiendi hivihivi bila dawa kuchimbwa…Pichani baadhi ya wasanii wakiwa wanachimba dawa njiani kurudi Dar baada ya show ya Fiest huko Dodoma..
29 Sep
Mhh kuna style na style jamani za kuiga…..
Binafsi napenda style ya nywele simple kwasababu tu napenda kuwa hivyo.
Kuna wengine wanapenda kwenda na fashion na kila kitu,ni vizuri lakini tuangalie na vya kuiga..
Kuna vitu vya kuiga na vingine tuache vipite tu kwasababu tunaweza kuonekana vituko…
Style kama ya huyu jamaa kwakweli mimi binafsi natupa kule,sio kwamba sijaipenda ila style na mtu mwenyewe ni vitu viwili tofauti na ndiyo maana wakati mwingine tunashauriwa kuwashirikisha watu ili kuweza kutushauri.
29 Sep
Hivi umewahi kujiuliza kwanini unatoa chozi?!
Inawezekana una furaha au umekerwa na kitu fulani au kitu chochote kile na unajikuta unadondosha chozi…
Swali ni je,ni kitu gani hasa kinachoweza kukusababisha wewe ukadondosha chozi?!
29 Sep
Imeanza na mkoa wa Dodoma na wiki hii siku ya Jmos Fiesta inaelekea kule jijini Arusha.
Kwa taaarifa tu ni kwamba Pipi na Barnaba,Ngwear,Belle 9 na vichwa vingine vilivyosababisha pande za Dodoma.
28 Sep
Mr blue aka Young Babylon toka Micharazo adondosha nyingine baaada ya tabasam kufanya vizuri sana katika anga ya music hapa bongo,ngoma hiyo mpya inaitwa ‘TUKO PAMOJA’ akiwa na nemo,aliyewahi kuwa ndanik ya Wakali Kwanza.
Baada ya kudondosha mawe hayo mawili kinachofuata ni albam kutoka kwa Bluee..Lets wait what hes going to bring..
25 Sep
Inasemekana dawa ya gonnjwa hatari la ukimwi imepatika..Kwa anaejua zaidi abainishe kama habari hizi ni za kweli au ndio rumours tu!
25 Sep
Mashindano ya kumtafuta Mrembo wa Tanzania yapo mbioni kufanyika na kipindi hiki warembo wapo kambini..
Nisieleweke vibaya kuwa napinga kitendo ambacho nataka kuongelea.
Siku za nyuma,mkufunzi wa dansi wa mashindano haya alikuwa ni msanii wa nyimbo za kiutamaduni nchini Wanne Star ambaye alikuwa anawafundisha style nzuri na zilikuwa zinavutia sana..
Mwaka huu habari ni kwamba anafundisha Sammy Cool ambaye aliweza kutingisha sana miaka hiyo kwa kucheza miondoko ya MJ….
Tatizo nalotaka kuliongelea hapa sio kubadilishwa kwa walimu hawa wa dansi bali ni kwa WAREMBO wa mwaka huu kufundishwa jinsi ya kucheza kama Marehemu Michael Jackson….
Kumbuka ni mashindano ya kumtafuta mrembo wa Miss Tz,na inakuaje warembo wafundishwe kucheza kama Michael Jackson na sio kufundishwa kucheza nyimbo za Kiafrika au hata nyimbo za utamaduni wa kwetu???
PICHA KWA HISANI YA ISSA MICHUZI.
25 Sep
Baada ya siku chache habari kusikika kuwa TID anatarajia kuoa baada ya mfungo wa ramadhani,mwenyewe aibuka na kusema kuwa hapendi kuzushiwa kwkauwa habari hizo si za kweli.
“Kwakweli hakuna kitu ninachochukia kama kuzushiwa kitu ambacho si kweli,kuoa baada ya mwezi wa ramadhani ni habari za uzushi mtupu”
Mbali na hayo alikiri kuwa mpango wa kuoa anao na anatarajia kufanya hivyo mwisho wa mwaka huu!!
25 Sep
Ile nyimbo ‘Violet’ ya matonya iliyotamba sana katika anga za music wa bongo mwaka mmoja nyuma hatimaye siri yagundulika.
Msanii khalid tunda au muite Tundaman kutoka Tip Top connection alithibitisha maneno hayo kwa kusema kuwa ile ngoma ya ‘Violeth’ alikiandika yeye na vibao vingi tu kwa wasanii mbalimbali lakini baada ya kuona hakuna faida yoyote anayoipata kutokana na kazi hiyo ikiwemo hata kutajwa kuwa ye ndio mwandishi,akaona bora aingie kwa fani hii na kuanza kupiga kazi ili ulimwengu umjue !!
Recent Comments