
Banza Stone mwana wa Masanja achonga na Angaliabongo na kudai kuwa yupo fiti na atarudi hivyo mashabiki wake wasichoke kumsubiri. Haya ni maswali mafupi aliyohojiwa na Angaliabongo.
Angaliabongo: Banza mashabiki wako wanakuuliza upo wapi na unafanya nini?
Banza: Nipo ila kuna mambo fulani yalikuwa yananiweka vibaya ila siku si nyingi nitaweza kusikika tena na mashabiki wangu.
Angaliabongo: Vipi madai ya kuwa unaumwa na uzushi wa kifo?
Banza: Kwakweli ndio maana naitwa Makaveli kwakuwa kila siku nazushiwa kifo lakini kama unavyoniona,mimi ni mzima wa afya njema.
Angaliabongo: Banza unasumbuliwa na nini hasa kwasababu tunaona tu kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuwa unaumwa,nini hasa kinachokusumbua?
Banza: Nasumbuliwa na kichwa pamoja na malaria na si kinginecho.
Angaliabongo: Je mashabiki wako wategemee nini kutoka kwako?
Banza: Wategemee kitu special,nitatoa wimbo maalumu kwa wale wote wanaonisema vibaya.
Angaliabongo: Asante Banza
Banza: Asante!
Related posts:

banza, nakuombea upone mshikaji. Mungu mkubwa na anakusikiliz katika sala zako za kila siku. Tulizana upone na usiwe na kinyongo na wanaokusema. mashabiki tunakusubiri sana urudi ili tupate kusikia tungo za nguvu. Mungu akulinde.
da kaka pole sana mwanangu nakuonea huruma kinoma ili watu wasikuandame mno kuwa unaumwa huu ugonjwa wa kisasa pima wka majibu hadharani mwana itakusaidia ile mbaya sie huku ughaibuni malaysia m2 akizushiwa anaweka majibu hadharani wa2 wana2lia
pole sana banza ila je utarudi kwenye gemu wa staili gani nina maaana unrudi na bambino au unatokea fm academia? karibu kwenye tena uraiani
hi banza
niefurahi kusikia kwamba u-mzima chamuhimu usijibu nyimbo za mashambilizi wewe imba wimbo ambao kila mtu akiusikia atanyanmaza kimya sababu uzima au ugonjwa wako ni mapito na pia ni maamuzi ya Mungu.Kila mtu analinwa na Mungu HIVYO YOA WIMBO WA SHUKRANI NA WA KUWAASA WATU JUU YA YALIYOKUSIBU kila mtu ni mgonjwa hata kama ni kicha pia nai ugonjwa.la muhimu toa kibao cha kujenag ana si kibao cha kubomoa maana kama utatunga wimbo wa kuwashambulia hapo utaamusha mengine
nakutakia kil laheri KAKA YANGU BANZA,
Anitha binti wa Yesu
hi uko juu sana nachokushauri usianze na majungu we fanya kazi niayo tu na tumekumiss mbaya