Angalia Bongo

Sehemu ya Kuwepo!

Archive for July, 2009

Ujambazi wa Mabomu leo Temeke.

Ni moja ya bomu lililotumika na majambazi huko Temeke leo asubuhi.

Ni moja ya bomu lililotumika na majambazi huko Temeke leo asubuhi.Habari na picha kwa hisani ya www.issamichuzi.blogspot.com damu ya wafanyakazi wa katika kaunta ya benki ya NMB tawi la Temeke ambapo majambazi yapatayo saba hivi yalivamia kwa mabomu ya mkono ambapo baada ya kurusha mawili nje na kuua mlinzi wa kampuni binafsi aliyekuwa getini, yakarusha risasi ndani na kujeruhi watu 13, ikiwa ni pamoja na askari polisi wawili na kukomba takriban shilingi milioni 150 kabla ya kutoroka. Walitoroka na Escudo na Prado zilizokuwa na namba za 'SU' na 'STJ'

  • 0 Comments
  • Filed under: Angalia Bongo
  • marem1
    Rapa Eminem anayetamba na wimbo ‘We made You’ aachia wimbo wa kumdiss Nick Canon na Mariah Carey.
    Kitendo cha rapa huyo kumuimba vibaya Mariah na Nick kimewashangaza watu wengi na huku wengine wakisema rapa huyo hana kazi ya kufanya…

    “Mariah and Nick… Please , do not respond. This is what this guy does for a living”
    Hebu ingia hapa kujua mengi kuhusiana na habari hii

    http://bossip.com/137305/eminem-rides-on-nick-cannon-and-mariah-carey-in-new-diss-track-that-goes-for-nick-too-fckin-fggot/#more-137305

  • 0 Comments
  • Filed under: Angalia Bongo
  • Nipo fiti…Banza Stone!

    banza

    Banza Stone mwana wa Masanja achonga na Angaliabongo na kudai kuwa yupo fiti na atarudi hivyo mashabiki wake wasichoke kumsubiri. Haya ni maswali mafupi aliyohojiwa na Angaliabongo.

    Angaliabongo: Banza mashabiki wako wanakuuliza upo wapi na unafanya nini?

    Banza: Nipo ila kuna mambo fulani yalikuwa yananiweka vibaya ila siku si nyingi nitaweza kusikika tena na mashabiki wangu.

    Angaliabongo: Vipi madai ya kuwa unaumwa na uzushi wa kifo?

    Banza: Kwakweli ndio maana naitwa Makaveli kwakuwa kila siku nazushiwa kifo lakini kama unavyoniona,mimi ni mzima wa afya njema.

    Angaliabongo: Banza unasumbuliwa na nini hasa kwasababu tunaona tu kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuwa unaumwa,nini hasa kinachokusumbua?

    Banza: Nasumbuliwa na kichwa pamoja na malaria na si kinginecho.

    Angaliabongo: Je mashabiki wako wategemee nini kutoka kwako?

    Banza: Wategemee kitu special,nitatoa wimbo maalumu kwa wale wote wanaonisema vibaya.

    Angaliabongo: Asante Banza

    Banza: Asante!

  • 5 Comments
  • Filed under: Angalia Bongo
  • R5T8H8_large
    Katherine Jackson ambaye ni mama mzazi wa Hayati Michael Jackson apewa haki zote za kukaa na watoto watatu wa Michael Jackson huku aliyekuwa mke,Debbie Rowe kuambulia patupu.

  • 0 Comments
  • Filed under: Angalia Bongo
  • Sexiest Man achukua chake leo

    3 copy
    Mo Rocka kijana aliyejishindia U-Sexiest man in Dar akabidhiwa kitita chake leo cha shilingi za kitanzania milioni moja kutoka Clouds Fm.

    Kijana huyo mwenye mvuto ashukuru sana Clouds na kusema kuwa anatumia kiasi fulani cha fedha hizo kwa watoto yatima.

    “Nashukuru kwamba nimekabidhiwa zawadi yangu na kuahidi kuwa nitatumia kiasi fulani na watoto yatima”Mo Rocka.

  • 0 Comments
  • Filed under: Angalia Bongo
  • Marlaw
    Msanii wa Bongo Fleva nchini Marlaw anayetamba na wimbo Peep Peep’ anatarajia kuachia albam yake ya pili mwezi ujao ambayo bado hajajua aipachike jina lipi.

    Akiongea na Angalia Bongo, Marlaw alisema kuwa albam hiyo itakuwa na jumla ya nyimbo kumi na mbili.

    “Sijajua jina la kuipa albam yangu lakini cha msingi ni kwamba mwezi ujao albam itakuwa mtaani na itakuwa na jumla ya nyimbo kumi na mbili” Marlaw

  • 1 Comment
  • Filed under: Angalia Bongo
  • Kunguru weusi marufuku Dar.

    .lukuvi

    Kunguru weusi waliotapakaa jijini Dar-es-salaam wamepigwa marufuku jijini Dar-es-salaam kwakuwa wameonekana kuwa ni waharibifu na wanahatarisha maisha ya binadamu na wanyama.
    Akiongea na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-salaam,William Lukuvi alisema kuwa hapo mwanzo kunguru hao walipelekwa Zenji (Zanzibar) kwa lengo la kula wadudu waliokuwa wanaharibu zao la karafuu visiwani humo lakini tatizo linakuja kuwa wanazaliana kwa haraka bila mpango wowote na sasa wanafanya uharibifu katika maeneo mbalimbali ya mji.
    Kutokana na hilo Mkuu huyu wa mkoa ameomba kwa mtu yeyote mwenye uwezo wa kuwaangamiza kunguru hawa afanye hivyo kwasababu ni waharibifu wakubwa

  • 0 Comments
  • Filed under: Angalia Bongo
  • Vote for MwanaFa & AY

    n783400149_6469876_1643593

    Tanzanian Bongo Flava artist Hamis Mwinjuma aka MwanaFA has been nominated by Channel O Music Awards Which is gonna be held in Johannesburg South Africa on 29th October 2009,

    His video track name NAONGEA NA WEWE featuring AY has been nominated into two categories.The Most Gifted Group (DUO) and The Most Gifted East African Video.

    MwanaFa and Ay they begging you to vote so as they can win awards.Its obviously they can,and by winning this they’ll put up Bongo flava to the map.Take your time and remember you are vote for our country and our musics.
    HOW TO VOTE

    To vote, MWANAFA The Most Gifted or Duo must SMS 4E to +27839208400

    To vote, MWANAFA The Gifted East Africa Video must SMS 13B to +27839208400 (International SMS rates apply)
    or vote on http://www.channelo.tv (web). Is where you can vote

    You can vote as many as you want!

    Regards;
    MwanaFA & AY…

  • 0 Comments
  • Filed under: Angalia Bongo
  • Tumeshindwaje kudhibiti ukahaba?

    prostitute
    Nchi yetu ni moja kati ya nchi zinazokabiliwa na tatizo la ukahaba..Tutawezaje kudhibiti ukahaba nchini?
    Kuna kipindi niliwahi kutembelea mkoa wa Dodoma na nilisikitishwa sana kutokana na kuona watoto wadogo wakiwa tena umri chini ya miaka kumi na nane wakiuza miili yao…Hapa tufanye nini ili kuweza kudhibiti hali hii?

  • 0 Comments
  • Filed under: Angalia Bongo
  • Mapokezi yaMuungano mzuxx

    fella

    muunganiko wa machama makubwa mawili ya tmk na tip top connection unaendelea kufanya maangamizi ile mbaya katika mikoa kadhaa ya tour yao,wameanza na sumbawanga wakaja mbeya na kesho watakua iringa wakitambulisha album mpya na nyimbo mpya kama ya madee pesa,album kama za temba fella na 2ndaman na spark,wamepokelewa kwa shangwe kubwa kila wanapopiga ngoma zao kwa stage,kweli kazi ipo mkubwa na wanawe huku abdu bonge na washkaji

  • 0 Comments
  • Filed under: Angalia Bongo
  • About Angalia Bongo

    Hey how you doing DEAR fan! Thanks for passing By in my world...I would apreciate İf you can call me SARAH, was born in the middle of 80’s.. By proffesion a journalist and always straight with my desicions, without forgeting İ enjoy life to the fullest and always believe in Jesus, Remember İm a pure Christian.Love friends and believe to DİE with something as İ was born with NOTHİNG…İ think thats to much to know about me. Thanks for passing by xoxox..... Read More

    Have Your Say

    How Is our Website?

    View Results

    Loading ... Loading ...

    GrooveBack



    Disco bora na la kijanja nchini, pekee linalowahusisha waliokuwapo, waliopo na wanaotaka kujua kilichotokea