Sehemu ya Kuwepo!
29 May
28 May

Mashindano ya urembo ya kumsaka kisura wa kitongoji cha Kigamboni 2009 kupitia Kampuni ya Bongo5 Media Group,imefikia ukingoni kwakuwa mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika siku ya jumamosi ya May 30 kwenye ukumbi wa Maeese Beach Resort zamani Hunters beach Kigamboni.Washiriki mbalimbali wamejitokeza kushiriki mashindano hayo na mpaka sasa jumla ya walimbwende 11 watachuana vikali kuliwania taji hilo la Miss Kigamboni 2009,aidha katika mashindano hayo burudani itapambwa na THT Odama band,Mwasiti,Maunda Zorro,Barnabas pamoja na Pipi.
27 May
Kwa jina anakwenda kama Nurdin ila wengi wanamfahamu kama Scheta au Soulja Boy wa Bongo..Huyu ni msanii chipukizi kabisa anayetamba na ngoma ya ‘Wadhifa’ aliomshirikisha Noorah na Richard…Anasema anamzimia sana Soulja Boy na ndiyo maaana muonekano wake upo kama Soulja Boy Tell Em……..Mpango wake wa baadaye ni kufikia anga za kimataifa na kuweza kufanya ngoma na Soulja Boy.
26 May
Hii ilikuwa ndani ya kichwa changu na nimeamua kukiweka hapa ili wadau muweze kushare na mimi mtazamo huu juu ya wasanii wetu wa hapa nyumbani.
Inasikitisha sana kuona msanii anakuwa kama maji yani kupwa na kujaa,Unajua namaanisha nini?Kuna kipindi unakuta msanii flani anatamba sana kwenye redio,magazeti na kila sehemu kutokana na single yake ambayo imepokelewa vizuri na jamii na kuweza kupendwa lakini baada ya muda jina la msanii huyo linafifia hata msanii mwenyewe kupoteza dira kabisa….HII INATOKANA NA NINI?
Kwa mtazamo wangu,wasanii wajihusishe na shughuli mbalimbali za jamii ambazo nafikiri zingeweza ku-maintain majina yao kwenye jamii yetu na kuachana na pombe,uzinzi na madawa ya kulevya..
Kwa mfano halisi…mastaa kibao na wengi wao wa nje mbali na kuimba au kucheza movie wana kuwa na kitu fulani ambacho kina-maintain jina lake kwenye jamii na watu wanapata kumsikia…
Jay Z pichani alikuja nchini kama balozi wa maji,kama sikosei na alienda Mwananyamala Hospitali kuzindua kisima cha maji safi..Tumeweza kuona Kelly Rowland kama balozi wa Ukimwi na alizuru nchini na kuzama mpaka Uwanja wa fisi,Yvonne Chakachaka kutoka nchini Afrika Kusini kama balozi wa Malaria,Anjela Jolie anahusika na mambo ya UNICEF na wengine wengi tu lakini kwanini wasanii wetu nchini hawafikirii kuhusu hilo na wanaishia kusema Game ya Bongo imejaa ushirikina na maovu mengine na wakati ukweli unaonekana kwamba wenyewe hawajishughulishi?Inasikitisha sana….Ushauri kwa wasanii wote ambao ni wa bure kabisa,wafikirie kufanya kitu fulani katika jamii ambacho kitaweza kuweka majina yao on Top…
Hongera kwa Moracka ambaye yeye pamoja na gazeti la Bang alijitolea kwenda kwenye vituo vya watoto yatima na kutoa misaada mbalimbali……Kwangu mimi naona nimelifikisha mezani,wadau changieni mtazamo huu
26 May
26 May

Wasanii wawili waliokuwa ndnai ya TMK …Rich One, na Baba Levo…wameamua kutoka kivyao na albam ya pamoja waliyoipa jina la KAMAKAWA.
Taarifa kutoka kitaa cha TMK….albam hiyo yenye nyimbo 8… imefanywa katika studio tofauti tofauti ambazo ni Bongo Records chini ya P.Funk, Fish Crub chini ya Producer Lamar na Tongwa Rec chini ya Producer Duke.
24 May

kundi la wanaume tmk family lililo chini ya usimamizi wa said fella
24 May

mwanadafada ray c ameibuka na kusema kuwa habari za uzushi zilizoenea mitaani kuwa wameachana ni uongo mtupu kwani wanatarajia kufunga ndo hapo mapema mwakani,ray c alisema piaanatarajia kuacha music ili ajishugulishe na biashara zake nyingine kwani ameona music industry ya kibongo iko na mizinguo kibao hivyo soon ataachana na mambo ya music na kufanya shughuli zake binafsi,kila la kheri lord eyez na rehema chalamila
24 May

wadau hiki ndio chanzo cha habari,kwa style hii imani za kishirikina zinawezekana kabisa zikawa zinatumika,shimo hili na gari alilokua nalo mhehimiwa naamini unaweza pita hata na speed 120 na gari ikatingishika tu,wadau hii ndio bongo dar es salaam,ridhiki ya mtu mikononi kwa mtu,tuatafika kweli
24 May

mbunge wa kyela mheshimiwa H.Mwakyembe hatimaye apata nafuu baada ya kupata ajali maeneo ya iringa akiwa na gari lake binafsi,mwakyembe alisema ajali hiyo ilisababishwa na shimo dogo lililopo barabarani ambapo kimuonekano ni dhahiri haliwezi kusababisha ajali mbaya kiasi kile,mheshimiwa alisema ni mbinu tu za wapinzani kutaka kummaliza lakini kwa rekhma za mnyaaz mungu leo yu hai,hivi kweli imani za kishirikina zinaaminiwa hata na wasomi?wadau nipeni jibu
Recent Comments