Sehemu ya Kuwepo!
29 Apr
This is a step by step of how Kenya’s celebrity couple Wahu and Nameless, quickly made up after a mini-second altercation on the dancefloor. This incident took place at Blue Times Lounge, Museum Hill during the MTV Africa Music Awards (MAMA) party a while back
What happened was, Wahu found Nameless dancing with Nike Kondakis – the chic who designs dresses from used and old parachutes.
Wahu went over to him and whispered something in his ears after which the paps started clicking away. After, some push and shove the celeb couple, Wahu and Nameless posed for the paps. Crisis Averted. Period. 
How it ENDS
29 Apr
Mabomu yalipuka huko mbagala kizuiani kwenye kambi ya jeshi
Watu watatu wafariki dunia na majeruhi kibao wakimbizwa hospitali ya temeke.
Watu mbalimbali wafurika hospitalini kuona ndugu zao
Sina la kusema wadau.Hali ilisikitisha sana..Kama unavyoona vipande vya mabomu
Hiyo ndiyo hali halisi.Chanzo kinasema mabomu yalipata joto sana iliyopelekea kulipuka.
28 Apr

Msanii wa muziki wa r&b nchini Maunda Zahir Zorro ameibuka na kusema huu ni wakati wake wa kutoa albam yake ya kwanza.
Maunda aliyezaliwa katika familia yenye vipaji, alisema kuwa amekaa kimya kwa muda mrefu hakutaka kuzungumzia kuhusu ujio wa albam yake kwa sababu maalum.
‘Nilikuwa kimya kwa muda mrefu, sijawahi kutoa tamko lolote juu ya albam yangu zaidi ya kutoa nyimbo tu, kwa kuwa sikutaka kutoa ahadi hewa, lakini sasa nataka kuwaambia mashabiki wangu wakae tayari kila kitu kipo tayari na muda si mrefu wategemee kupata albam yenye ubora wa hali ya juu’ alisema Maunda.
Maunda ambaye amewahi kutamba na vibao vyake ‘Niwe wako’, na ‘Mapenzi ni ya wawili’, amefanikiwa kuwika katika chati ya juu ya wasanii wa kike nchini.
Maunda ni zao la THT na mmoja wa wasanii wakali kwa sasa katika muziki wa kizazi kipya.
28 Apr

Msanii Sumalee ambaye alikuwa akiunda kundi la Packlane la mjini Tanga wiki hii ameibuka na kusema kuwa bado yupo ngangari kwenye gemu.
Park Lane ambaye alitamba sana mwaka 2001, ameutambulisha wimbo wake mpya uitwao ‘Ndani ya Week’.
Kutokana na kimya kirefu hapa kati, jamaa alisema kuwa kimya chake hakikuwa cha kawaida kwani alikuwa chimbo akifanya mambo mengine na sasa amerudi rasmi kwenye game.
Akiongea kuhusu ujio wa album yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Hesabu za Mapenzi’ alisema kuwa yuko mbioni kukamilisha album hiyo na atawatangazia ni lini hasa album hiyo itakuwa sokoni.
“Kwa kuanza nataka wapenzi wangu waangalie video na kusikiliza wimbo wangu huu kama utambulisho, naamini ni ujio wangu mpya na nataka kuwahakikishia kuwa nakuja kikweli wapenzi na washabiki wangu wakae mkao wa kula” alimaliza Suma Lee.
28 Apr
Baada ya kutoka na ‘Bila Yule’ na kuukamata muziki wa kizazi kipya kwa muda, sasa kijana Abraham Mkasembe a.k.a Dulayo yupo chemba akiandaa albamu pamoja na mkongwe wa muziki wa r&b anayefahamika kama Joslin.
Dulayo ambaye alishaanza kuonekana kukaa kimya na wengi kuona kama ameishiwa, amesema kuwa kutokana na wengi kuwachanganya katika staili za uimbaji pamoja na sauti zao wameonelea ni vema kama wakifanya kazi pamoja.
“Tumekaa pamoja na kujadili, kutokana na staili zetu kufanana tumeona ni vizuri kama tukifanya kazi pamoja ili kuweza kuleta uwiano ulio bora pamoja na kazi nzuri pia” alisema Dulayo na kuongeza kuwa tayari wameshaandika baadhi ya mashairi na wapo mbioni kuanza kurekodi.
Dulayo ni msanii ambaye alianza kutamba na kibao cha Utamu ambacho kilirekodiwa na prodyuza Marco Chali, ‘Bila yule’ mwaka 2007 mwishoni alichomshirikisha Mwana FA.
28 Apr
Tumesikia tuzo mbalimbali kama za wanamuziki nchini,za waigizaji na sasa kwa mara ya kwanza kampuni ya PTECHS inakuletea Tanzania Academic Award,maalumu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari waliofanya vizuri.Mitihani ilikuwa tarehe kumi na nae mwezi huu na tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa mwezi ujao tarehe 23 na wasanii mbalimbali kama Makamua na QJ,Profesa Jay,Spack na Tundaman pamoja na kundi zima la Bongo Dar-Es-Salaam wanatarajia kusindikiza uzinduzi huo utakaofanyika viwanja vya leaders!
Akielezea kuhusu utoaji tuzo huo,Msemaji wa PTECHS, Godfrey Maginga alisema tuzo hizo ni maalumu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari na wao hasa wamelenga elimu na ndiyo maana kampuni hiyo imeamua kuandaa kitu maalulmu kwa wanafunzi kwakuwa wanaonekana kama hawapewi changamoto yeyote kwenye elimu.
28 Apr
Hii tuite nini wadau?Kila mtu anakula kazini kwake au inakaaje kaaje hii?
Kama picha inavyojielezea,hapo ni maongezi ya dereva na trafiki amevuta mkwanja wake.Kile kitu tunachopinga kila siku na mpaka tume zimeundwa kitaisha lini Wadau?
24 Apr

Mwanamuziki wa bongo Flava anaetamba na wimbo ‘Pip Pip’ Marlaw amedai kwamba wimbo huo aliuachia baada ya kuona kero ya foleni barabarani na ndio maana aliamua kutunga wimbo huo wenye meseji ya ya kuchelewa kufika kweny apointment aliyopanga na mpenzi wake baada ya kukaa muda mrefu kwenye foleni…
“Afrika mashariki kwa ujumla tunakero kubwa ya trafic jam na kuona kwamba hiyo ni kero kubwa niliamua kutunga wimbo huu”Marlaw…
23 Apr

IKIWA ni miezi michache tokea mkali wa hiphop BONGO,Chid Benz kutangaza kuacha music,rapa huyu aibuka na kusema albam yake inadondoka mtaani so soon ila mpaka sasa hajui ngoma gani iingie kwenye albam hiyo ya ‘The Return Of The Big Boss’ kwakuwa ana jumla ya nyimbo 27 na zote ni kali..
23 Apr

Huyu ndiye Miss Tz wa kwanza aliyepata ushindi mwaka 1967 ambaye alifariki dunia january 26 mwaka 2007 na maradhi ya kansa ya tumbo huku akiwa na umri wa miaka 61..Kuna haja kubwa ya kumuenzi kama balozi wa kwanza kuiwakilisha TZ kwenye mashindano ya Urembo duniani.
Picha kwa hisani ya Darhotwire
Recent Comments