
Kampuni ya Bongo 5 ni moja ya kampuni yenye kushughulika na mambo ya kuandaa matamasha mbalimbali hapa nchini.
Mwaka huu imeamua kuandaa mashindano ya Miss Kigamboni ambayo yanatarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi wa nne.
Mratibu wa mashindano hayo ambaye ndio mkurugenzi wa Bongo5,Luca anasema ya kwamba mashindano ya mwaka huu ya kumtafuta mrembo wa Kigamboni yatakuwa ya aina yake kwakuwa wamejipanga vyema na wanaamini kwamba mwaka huu lazima Miss Tanzania atokee Kigamboni.
Mwaka huu tumepania kumtoa Miss Tanzania kutoka kitongoji cha Kigamboni na kuandika historia ya kwanza kwa Miss Tanzania kutoka Kigamboni,washiriki wanaombwa kujitokeza kwa wingi kwani zawadi za mwaka huu ni bab kubwa”Alisema Luca.
Mbali na hayo form za kushiriki kwenye mashindano hayo zinapatika kwenye ofisi za Bongo 5 zilizopo Posta karibu na club Billcanas
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na
+255786009009
+255786712222
+255713946403
Related posts:
