Sehemu ya Kuwepo!
24 Feb

Zoe Saldana na mumewe Oscar Steez,wapo na wanaendelea kuishi pamoja.Ndoa yao ina miaka themanini na nne…na bado wanadunda,wewe je?
23 Feb

Mshiriki wa Big Brother mwaka 2002 afunga ndoa maalumu ya watu mia mbili hiyo baada ya kujua kwmaba ana siku chache za kuishi duniani baada ya kansa kumuenea mwili mzima.
Jade mama wa watoto wawili mwenye miaka ishirini na saba anafurahia siku hizo chache alizobakisha hapa duniani kabla ya kifo chake.
23 Feb

Wali Nazi wa Jaffarie kutoka Wateule upo tayari mzigoni na watu wameupokea vizuri.Mwanamuziki huyu wa siku nyingi ameachia video wiki iliyopita na kila kona wanaizungumzia kutokana na jinsi video ilivyo bomba na Meseji wa wimbo huo…Jafa yupo mzigoni kuachia albam baada ya kuwa resi na project yake ya mwaka 2009 ndani ya studio za Fishcrab ya Lamar
23 Feb

Shirikisho la wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya yaani Bongofleva linaloitwa (Tanzania Flavour Unity) limeanzishwa na tayari limekwishapata viongozi wake katika mkutano uliofanyika wiki hii siku ya jumatano katika viwanja vya Leaders Club.
Katibu mkuu wa shirikisho hilo ambaye amechaguliwa kwa sasa mwanamuziki na kiongozi wa bendi ya B. Band Banana Zorro, amesema mkutano wao ulifanyika vizuri na ulihudhuriwa na wanamuziki kadhaa walioitikia wito wa mkutano huo na kwa kuanzia wajumbe wa mkutano huo walichagua viongozi watakaoongoza shirikisho hilo kwa sasa.
Aliwataja viongozi waliochaguliwa na kuongoza shirikisho hilo na vyeo vyao kuwa ni Lady Jay dee ambaye alichaguliwa kuwa Mwenyekiti, TID alichaguliwa kuwa makamu mwenyekiti, Banana Zorro alichaguliwa kuwa Katibu mkuu, Jay Moe alichaguliwa kuwa Msemaji wa shirikisho hilo, amesema katika mkutano huo waliazimia kufanya vikao kila wiki ili kuhakikisha kuwa mipango yao inakwenda kama ilivyotarajiwa.
Banana alisema lengo la kuunda shirikisho hilo ni kutekeleza baadhi ya mambo ambayo yanatakiwa kufanywa na shirikisho hilo ili kujiweka sawa kwa ajili ya kupokea msaada mkubwa ambao Mh. Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete ambaye wanamchukulia kama mfadhili wao mkubwa aliahidi kuwasaidia wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya ambapo aliahidi kujenga (Mastaring Studio) kubwa ya kisasa kwa ajili ya kufanyia muziki huo Mastaring hapahapa nyumbani ili uweze kuendana na soko la kimataifa.
22 Feb

Picha hii ya Rihanna imezua utata mkubwa baada ya polisi kuitoa bila idhini ya Baba mzazi wa Rihanna ambaye hakutaka picha hii ionekane na vyombo vya habari.Hivi ndivyo Rihanna alivyoharibiwa na Chris Brown,lakini hali sasa inasemekana ni shwari kwa Rihanna.
20 Feb

Baada ya kuingiza sokoni nyimbo yake ya Nini Sina aliyomshirikisha mkali wa Hip Hop Bongo Chid Benz Stara Thomas mmoja wa wakongwe wa muziki hapa nchini amesema sasa ni wakati wa Album nzima kuingia sokoni.
Amesema kazi kubwa ya album hiyo imekwisha kamilika kilichobaki ni umaliziaji wa vitu vidgo vidogo tu ambapo anategemea kabla ya mwisho wa mwezi huu itakuwa imeingia sokoni tayari.
Stara ameongeza kwamba sambamba na hilo pia sasa hivi anaendelea na programu ya kurekodi Video za nyimbo zake tofauti tofauti katika kuikamilisha na kuiweka ubora wa hali ya juu album yake hiyo ambapo amesema nazo hazitachukua muda mrefu zitakuwa tayari kwa kusambazwa kwenye vituo vya Televisheni.
Album hiyo itakayokuwa na nyimbo sita ndani yake kuna wakali kama Ngwea. Q Chillah Alikiba na Chid Benz.
20 Feb

MER LARAIN Classic saloon iko mbioni kufunguliwa jijini bongo utapata wataalam wa kuzitunza na kuzitengeza kucha zako baada ya malalamiko mengi kuwa watu wengine wanapo weka kucha bandia kucha zao huoza au kuaharibika sasa usijali ufumbuzi wa tatizo lako upo njiani.Hebu pata maelezo zaidi kwa kutembelea http://comfidence.blogspot.com/
19 Feb

Breaking News jamani wadau,yule mmoja wa washitakiwa wanaokabiliwa na kesi ya gharama za majengo pacha,Amatus Liyumba atoweka na hajulikani alipo baada ya kuwepo nje kwa dhamana.Siku ya leo alitakiwa kuwepo mahakamani lakini hakutokea na badala yake,wadhamini wake wawili wamewekwa rumande mpaka mshitakiwa apatikane.
19 Feb

Huyu ni Rah P kwa wasiomfaham…alitamba sana na ‘Hayakuhusu’ ambao ulimuweka vyema kwenye gemu hapa Bongo.lakini cha kushangaza baada ya wimbo huo amekuwa kimyaaaa….yupo wapi kwa wanaojua?
19 Feb

Huyu ni Prezzo au unaweza kumwita Cash Money Brother(CMB) kutoka kule pande za Kenya…unaikumbuka ile ‘Nipe Nikupe ya Ay?basi alimshirikisha huyu CMB.Sifa yake moja kubwa ni kujisifia kwamba ana hela na hakuna kinachomshinda kununua popote pale…Enzi zile za raba za G-Unit kutoka,yeye ndiye alikuwa mtu wa kwanza kuzivaa kutoka hapa Afrika Mashariki kama inavyodaiwa na ilikuwa ni raba original kutoka G-Unit.Mbali na hilo kipindi Alicia Keys alivyodondoka nchini Kenya,Prezzo alitoa gari zake tano za gharama aina ya lexus kwa ajili tu ya mapokezi ya mwanadada huyo na akaomba kutoka nae out,lakini bahati mbaya alimtolea nje…
Recent Comments