Sehemu ya Kuwepo!
29 Dec
Ni Lamar Lambashy..mtoto wa kwanza kabisa kutoka familia ya Mzee Lambashy.Kipaji chake kilianza kuonekana akiwa na Majani,aka P-Funk.Kwa mujibu was Lamar anasema kwamba Majani ndiyo aliyeweza kuinua kipaji chake.Baada ya kukaa na Majani,akaamua kwenda pande za Mandugu Digital ambapo hakuweza kukaa sana na sasa navyokuletea habari hii,Lamar ana studio yake binafsi inayoitwa ‘FISHSCRUB’ na kashatengeneza ngoma kibao…..
29 Dec

Hali halisi ndiyo hii,ni daraja moja maeneo ya Mabibo likiwa kwenye hali hiyo.Kuna mbunge wa eneo hili lakini hali ndiyo hii…
29 Dec

ni club bilcanas,inafunguliwa mkesha wa mwaka mpya,jamani inavutia sana na nina uhakika kwamba ni club bora kabisa hapa nchini kwa hatua iliyofikia.
23 Dec
17 Dec
17 Dec
wazee wakimenya njegere na baadaye kuziuza zikiwa tayari zimeshatolewa maganda yake,ilikuwa ni mitaa ya kariakoo sokoni.
17 Dec
Dumu moja la maji lilikuwa linauzwa mpaka shilingi elfu mbili za kitanzania,hali ilikuwa mbaya ila jana maji yameanza kutoka tena,hii ndio angaliabongo!
16 Dec

Mwanamuziki wa bongo fleva nchini,Dully Sykes,atamba kupagawisha wakazi wa Dodoma kwenye tamasha lililopewa jina la ‘Usiku wa Kujiachia na Ndovu’ siku ya tarehe 24,mwezi huu ambapo itakuwa siku ya mkesha wa krismas.
Wasanii wengine watakaokuwepo simku hiyo ni pamoja na Makamua,Mchizi Mox,Jay Moe pamoja na Ngwair.tutaonaaaaaaaaa,halaf tutakuletea kitakachojiri siku hiyo.Ila kama wewe mjanja,na unapenda starehe,unaweza ukazama pande za Dodoma kuwa pamoja na Dully na wasanii wengine ili uweze kusababisha!
Kumbuka Usiku wa Kujiachia na Ndovu umeletwa na udhamini mkubwa wa bia uipendayo ya Ndovu Special Malt!!!!!!!!
16 Dec

Mwanamama Mbilia Bel anayependa kuonekana kwenye vivazi vya kihindi,anatarajia kutua nchini leo ambapo atakuwa na show pale New World Cinema pamoja na Fally Ipupa.Natarajia kuwepo…unakaribishwa,,,kiingilio ni shilingi elfu ishirini na tano yako tu…ukiwa ndani utapata dinner,drinks na mwisho unadondoshewa bonge ya show,hutakiwi kukosa.
14 Dec

mamboz!!hili ni onesho lililokusanya wanamuziki wa kizazi kipya nchini ambao ni Dully Sykes,Jay Moe,Mangwea,Mchizi Mox pamoja na Makamua na linatarajia kufanyika tarehe 24 mwezi huu ndani ya ukumbi wa ROYAL VILLAGE pale mkoani Dodoma.Zawadi mbalimbali zitatolewa kutoka kinywaji cha Ndovu Special Malt.Wakazi wa Dodoma ni zawadi maalumu kwao!wakae mkao wa kupokea vyuma hatari siku hiyo ya mkesha wa siku ya Chrismas.
Says SarahCo-ordinator
Recent Comments