Sehemu ya Kuwepo!
30 Nov

Inasemekana kwamba Ricco mshindi wa BBA3 kutoka nchini Angola alifuata nyayo za Richard na ndiyo maaana alitwaa taji hilo,na kama isingekuwa vinginevyo mchizi angeambulia patupu.
30 Nov

Hii ndiyo hali ya Chamillione,kwa habari bado anaendelea vizuri,tuna imani atapona na kuweza kumiliki jukwaa kama ilivyokuwa kawaida yake.Nikukumbushe tu chanzo cha kuumia miguu ni ndoto aliyoota kule mjini Arusha,ilimporomosha tokea ghorofa la tatu mpaka chini,kuja kustuka kavunjika miguu….
30 Nov
Unakumbuka miaka ya 2004 pale Mwanafa,msanii wa Bongoflava alitamba na wimbo ‘Ingekuwa Vipi?Basi hawa ndio waliomjibu ‘Ingekuwa Poa’.Kwa habari tu ni kwmaba Wandago wamepania kurudisha jina lao na kwamba albam ipo tayari na wanachotaka kuanza sas ani mvua za Ngoma kutoka kwao,wanasema hawajachoka kisanii,mambo ya shule yaliingilia kati ila sas wamerudi upya Sporty Thieves wa Bongo!
28 Nov

Disema Mosi,rais wa manzese,Madee aliyetamba na wimbo wa ‘Cheza Kidogo’ na ‘Hiphop Haiuzi’ anatarajia kutua ndnai ya Uingereza mwezi ujao tarehe moja.Wakazi wa huko kaeni mkao wa kumpokea Madee,rais wa manzese,anawaletea mambo ya Manzese!nahisi atakutana na Matonya na Kiba…..sina uhakika!
28 Nov

Wanamuziki hawa wa bongo flava waliotamba na wimbo wa ‘Habari Ndiyo Hiyo’ na ‘Nangoja Ageuke’ watazindua albam yao ya pamoja siku ya tarehe nane mwezi ujao,siku hiyohiyo,wanamuziki Fat Joe,Eve watatarajia kufanya show ndnai ya viwanja vya Gymkhana.
27 Nov

Yule mwanamuziki aliyetokea kung’ara mwaka jana na traki yake ya ‘Presha’ azushiwa kuugua ugonjwa wa kichaa tofauti anavyobainisha.
Hafsa alikubali kuumwa lakini alisema kwamba hakuugua kichaa na ilikuwa malaria ya kawaida.
“Nashangaa wameniambia kwamba nimeugua kichaa,sio kweli,nilikuwa naumwa malaria ya kawaida”Hafsa…
Hafsa mwenyewe kamaliza mzizi huu wa fitna kwa kusema kwamba akuwa anaumwa kichaa kama watu walivyosambaza habari hizo za kizushi!
27 Nov

Wanamuziki kutoka nchini,Mwanafalsafa,Joh Makini na Ngwear wanatarajia kupanda jukwaa moja na wanamuziki watakaokuja kufanya show mwezi ujao ambao ni Fat Joe pamoja na Eve.
Ni bahati ilioje kwa wanamuziki hawa kushare one stage na kina Fat Joe,I hope wataweza kubadilishana mawazo na kuweza kupata machache ambayo yatawasaidia!
27 Nov
Ijumaa ya tarehe 28,namaanisha ijumaa hii,bendi ya DIAMOND MUSICA INTERNATIONALE watawasha moto pale maeneo ya MANGO GARDEN,MWANANYAMALA kwenye tamasha maalumu litakalojulikana kwa jina la ‘USIKU WA SANDRA’ Onyesho hilo lenye nia kubwa ya kutaka kutambulisha baadhi ya nyimbo za bendi hiyo zitakazokuwemo ndnai ya albam ambayo itanarajia kutoka hapo mwezi wa kwanza mwakani litakuwa la aina yake kwakuwa maandalizi ya bendi hiyo ni makali sana. Rais wa bendi hiyo,Liver Hasan alisema kwamba siku hiyo wataweza kubainisha mapenzi hasa ni nini kwa kuyabainisha kwenye wimbo wao wa ‘MAPENZI KITU GANI’ Mbali na kuwa ni usiku malaumu wa kutambulisha nyimbo mbalimbali zitakazokuwa ndnai ya albam ya Diamond,vilevile usiku huo utakuwa ni maalumu kwa sarah peter: wa kutambulisha nyimbo mbalimbali zitakazokuwa ndnai ya albam ya Diamond,vilevile usiku huo utakuwa ni maalumu kwa bendi ya DIAMOND kuwaaga wapenzi wake kwa mwaka 2008 rasmi. Hutakiwi kukosa kwa wewe mpenzi wa bendi ya DIAMOND kwani kuna vitu vingi ambayo umeandaliwa na ambavyo naamini lazima vitakukosha kwakuwa mimi nilibahatika kuona mazoezi ya vijana hawa wakiwa kambini,kwakweli yanatisha,sasa sichukulii picha siku hiyo ityakuaje,nakusisitiza usikose,utakuwa unaidhulumu nafsi yako
26 Nov

Haya haya tena wale wenye vipaji ndoto ya kujaribu bahati yako kwa mwaka huu imetimia,kwa kuwa lile tamasha la Music Crossroads 2008.ambalo hufanyika kila mwaka barani afrika mwezi disemba limewadia linafanyika ijumaa katika ukumbi wa British council na jumamosi katika viwanja vya mnazi mmoja
Tamasha la Music Crossroad limekuwa na malengo zaidi ya kuwasaidia wanamuziki wanyumbani kwa kuwashindanisha na wanamuziki wengine kutoka nje ya nchi na kupata mshindi,na fainali safari hii itafanyika Zimbabwe.
Music Crossrod kama ilivyo kawaida yao hawachagui washiriki isipokuwa wameweka wazi kwa kila ambaye yuko tayari kushiriki katika tamasha hilo anaruhusiwa lakini kwa sharti maalum kwamba kila mshiriki atatakiwa kutumia vyombo au ala (Instrumental) na
siyo kuimba juu ya nyimbo.
25 Nov
waliowahi kuwa mawaziri nchini,Bazil Mramba pamoja na Daniel Lyona,wanashutumiwa kwa kosa la kutumia madaraka vibaya,na dakika hii navyokuletea habari hii,wapo rumande baada ya kushindwa kutekeleza yale waliyoambiwa pamoja na kutoa dhamana ya bilioni 3.9 hivyo kurudishwa rumande.Hapa naona sasa mambo yanaanza kuiva,Rais wetu JK ameamua kuwa muwazi na mkweli kutokana na harakati anazoziweka,moja ya yote ambayo ni kali ni kufufua maovu yaliyofanywa na viongozi wetu waliopita,Kazi Ipo!?
Recent Comments