Angeris Faber,mshiriki wa BBS ambaye yupo tayari kutuonesha kile alichonacho.Yupo mzigoni na anatarajia kuachia albam yake mapema ambapo tayari imeshakamilika.Tracks ndani ya albam hiyo ni pamoja na ‘Wewe’, ‘Mzuka’ ambacho kipo katika mahadhi ya ragga,’My Boo’, ‘Nataka sana’, ‘Stay with me’ na vingine.
‘Esterange’ ndiyo jina la albam hiyo. Na ukipenda kujua jina hilo
linamaana gani anasema; “ Hayo ni majina yangu mawili kwa pamoja, Ester na
Angie, ukiiskiliza albam hii wimbo wa kwanza mpaka wa tatu tu utakuwa
umepata maana kwanini nimeamua kuiita Mimi,”
Anatarajia kuachia video ya wimbo wake wa kwanza wa utangulizi, uitwao ‘Wewe’ akiwa amemshirikisha Chidi Benz ambaye ameamua kuonyesha kile alichonacho.

Related Posts

  1. "Hazibanwi Pua"
  2. Albam hazilipi-Dully Sykes!
  3. Albam yangu ni Modern Hiphop tuu-Nick wa Pili
  4. Marlaw kuachia albam ya pili mwezi ujao.
  5. Ujio Mpya wa Vicky Kamata