Sehemu ya Kuwepo!
30 Sep

Kwa wale wote watakaosheherekea sikukuu ya Eid kesho au keshokutwa,Eid Njema.HAVE A HAPPY EID,full of blessings from Allah…..
30 Sep

Superhead akiwa na Bow Lizzle!
Super Head,mwanamke anayefahamika kwa kudate na mastaa huko nchini Marekani inasemekana ya kwamba ni mjamzito na aliyempa ujauzito mrembo huyo si mwingine bali ni rapa Bow Wow ingawa Bow Wow hajatoa kauli yeyote kuhusiana na hilo..
Kwa habari zaidizaidi tembelea www.mediatakeout.com
29 Sep
29 Sep

Huyu ni mwanamuziki Cristian Bella kutoka bendi ya Akudo Impact ya jijini Dar-Es-Salaam,anatokea Demokrasia ya watu wa Congo,ametamba sana na kibao ‘Mapenzi ni Kitu Gani’.Aliwahi kusikika akisema live ya kwamba hakuna mtu yeyote anayemfikia kwa kuvaa vizuri kwa upande wa wanamuziki hapa Bongo.Mwanamuziki huyu amekuwa na majigambo ambayo yanasababisha aanze kupoteza Mashabiki.
Habari nyingine ni kwamba hapendi kushirikishwa kwenye nyimbo za wanamuziki wengine kwakuwa anaamini ya kwamba ana kipaji hivyo ni lazima atawafunika tu.Jamani,angaliabongo.blogspot.com kamwe haitoi habari za kidaku,kimbea wala kizushi,Haya maneno yalisemwa na Cristianbella mwenyewe na nikiwa kama shahidi nilisema ya kwamba ni lazima nilifikishe mezani ili wadau muweze kuchangia kuhusu hili…..
29 Sep

Kwa jina ni Kolo,huwezi kumkosa sehemu yeyote waliopo Akudo Impact.Kwenye sekta ya kucheza hashikiki mpaka ahakikishe kapata kitu!!ndio unaweza ukamtoa kwa steji ili mambo mengine yaendelee!
29 Sep

Ni mwanamuziki wa kibongo,Jose Mara kutoka bendi ya FM Academia akiwa na mwanamuziki kutoka nchini Uingereza,Blanchard De Plaizir wakishow love.Hakika mshkaji aliweza kumpa saluti Jose Mara kwakuonesha uwezo wake pale ndnai ya Msasani Beach hapo jana.
Hapo chini mwanamuziki De Plaizir akiwa ndani ya TBC alipoitwa kwaajili ya mahojiano
29 Sep

Mamodel wa Mahogany wakiwa wamevalia vivazi vya Ally Rehmtullah
Unacheki mzungu alivyopendeza ndnai ya kivazi cha Ally Rehmtullah?
Vivazi vya Ally Rehmtullah vikiwa vimevaliwa na model wa Mahogany kwenye fashion show ambayo imeweza kumpatia jina kubwa Designer wetu kutoka nchini,Ally Rehmtullah kwenye wiki ya fashion nchini humo!Ni designer mwenye umri mdogo sana lakini ameweza kupata mafanikio ndani ya nchi na sasa anaelekea kujulikana kimataifa zaidi.Kila la kheri Ally!
29 Sep
Mtikila kujitolea gani lakini ndugu yetu?
Alipigwa huko Tarime jamani wadau,alipoanzisha stori kuhusu Marehemu Wangwe,ndipo wananchi walipopata hasira!Wabongo ni zaidi ya noma…walimtoa mchakamchaka mpaka wakahakikisha wanamkamata na kumpa jeraha kichwani lililompelekea kushonwa nyuzi tatu.
29 Sep
Mwanamuziki wa miondoko ya Dancehall nchini,Mr Simple,aliyewahi kutamba na nyimbo zake kama ‘Mr Simple’ na ‘Father Of Dancehall’ arudi tena kwenye gemu na kuahidi kufanya makamuzi zaidi mpaka wabongo waweze kuelewa nini maana ya dancehall.
Akiongea na angaliabongo,Mr Simple alisema anatarajia kuachia track yake itakayoitwa ‘Nimestuka’ ambayo amemshirikisha Jackline mapema baada ya mfungo kuisha.
“Nimerudi kwenye gemu na naahidi kufanya mapinduzi halisi kuhusu muziki wa dancehall ambao unaonekana kupuuziwa sana hapa Bongo”Alisema.
27 Sep


Mkali wa miondoko ya rnb nchini,Makamua anayetamba na nyimbo kama ‘Hunijjui’ na ‘Why’ akiwa kwenye front ya magazeti ya nje akijiachia.
Recent Comments